Hatimaye Malawi imepata Rais mpya baada ya mivutano ya
kisheria kwa wiki nzima.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amesema kutoka mjini Blantyre
kuwa Profesa Peter Mutharika ameshinda uchaguzi huo kwa kupata asilimia 36.4 ya
kura zote akifuatiwa na Dr Lazarus Chakwera mwenye asilimia 27.8 huku Rais
anayemaliza muda wake Dr Joyce Banda akishika nafasi ya tatu kwa asilimia 20.2
na Atupele Muluzi amekuwa wa nne na asilimia 13.7
Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Mackson Mbendera amesema
uchaguzi huo ulikumbwa na changamoto nyingi lakini mwishowe nchi ni lazima
ipate kiongozi wake na kuwaomba wananchi kuwa na utulivu .
Kesi Mahakamani Awali Jaji Kenyata Nyirenda wa mahakama kuu
mjini humo jana usiku alitoa uamuzi kuwa hawezi kuvunja sheria kwa kuruhusu
tume iongeze muda wa kuhesabu upya kura kwenye maeneo yenye utata.Na kwamba
sheria inaitaka tume kutangaza matokeo ndani ya siku nane na si vinginevyo.
Uchaguzi wa Malawi ulifanyika Mei 20 nchini kote lakini siku
moja tu baada ya kupiga kura, malalamiko yakiambatana na mapingamizi ya
kisheria yakatawala kwenye mahakama kuu za Lilongwe na Blantyre.
No comments:
Post a Comment