Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, May 27, 2014

TAZAMA PICHA ZA BIBI WA KINAIJERIA ALIPOSOMEWA MSHTAKA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA UWANJA WA NDEGE DAR

 Mtuhumiwa alipofikishwa mahakamani hapo.
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) ya tuhuma za kukamatwa na madawa ya kulevya gramu 831.94 zenye thamani ya shilingi za Kitanzania milioni 37.4.
Mwendesha Mashtaka, Jackson Chidunda, alisema mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo,  Frank Mushi,  kuwa mshtakiwa anakabiliwa na tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya alipokamatwa  Mei 19, mwaka huu Cole akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipokutwa na madawa aina ya heroin. 
Baada ya kusomewa shtaka hilo mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa kuwa upelelezi haujakamilika. Kesi hiyo itasomwa tena katika mahakama hiyo Juni 10 mwaka huu na mshtakiwa amerudishwa rumande.
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment