skip to main |
skip to sidebar
Wanne mbaroni kwa kukutwa na silaha za kivita Mara
Jeshi la Polisi mkoani Mara, limekamata bunduki saba zikiwemo za kivita
pamoja na risasi 461 toka kwa watu wanne wakiwemo raia wawili wa nchi jirani ya
Kenya, ambao wanatuhumiwa kuhusika katika mtandao mkubwa wa ujambazi wa kutumia
silaha.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Ferdinand Mtui,
akizingumza na jana Mei 5, 2014, alisema watuhumiwa
hao walikuwa na bunduki moja aina ya SMG na risasi 23 silaha ambazo ni za
kivita na nyingine za moto zikiwa zimekamatwa na wananchi kwa kushirikiana na
Jeshi hilo katika oparesheni inayoendelea katika mkoa huo.
Hata hivyo, amesema watuhumiwa hao wakitokea katika Wilaya ya Tarime wakiwa
na silaha hizo ambazo walikuwa wamezificha katika tenga lenye
ndizi mbivu wakiwa tayari wamefika mjini Musoma kwa ajili ya kufanya
uhalifu.
Amesema baada ya kukamatwa watu hao walianza kupigwa na wananchi kabla ya
Polisi kutumia nguvu kwa kurusha risasi hewani na kuwatawanya wananchi hao, kwa
ajili ya kuwakoa na kwamba wawili kati yao wamekufa wakati walipokuwa
wanapelekwa hospitali kupatiwa matibabu kutokana na kipigo walichopata kutoka
kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment