Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP
Na: Sylvester Onesmo
wa Jeshi la Polisi Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa
wa Dodoma linawashikilia watu 34 wakazi wa Mji mdogo wa Kibaigwa Kata ya
Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu
mali tukio lililotokea tarehe 05/05/2014 majira ya saa 13:30Hrs.
Kamanada wa Polisi
Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP
amesema Vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya miatatu wakishirikiana na Wabeba
mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa, walifanya maandamano bila kibali na
kung’oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa lenya tangazo la kutoruhusu
wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa
sheria. Viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu tarehe 01.07.2013
ambapo gunia la Kg. 100 za karanga zilipanda kutoka Tshs. 1000/= hadi Tshs
3000/=, guina la mahindi lilipanda kutoka Tshs. 500/= hadi Tshs. 1000/=, dumu
la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Tshs. 500/=, gunia la mashudu lilianza
kutozwa Tshs. 1000/=, gunia la alizeti lilianza kutozwa Tshs. 1000/= ushuru
ambao unapingwa na wabeba mizigo.
Vijana hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga
barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma mataili, pia walivamia
maduka na bar za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.
Kamanda MISIME
amesema katika vurugu hizo walisababisha uhalibifu wa mali kwa kushambulia
magari kwa mawe likiwemo gari la Mbunge wa Tanga Mh. OMARI NUNDU lenye namba za
usajili T.419 CWC Land Cruiser Prado ambaye aliyekuwa akienda Bungeni Dodoma,
pia gari la Polisi namba PT. 0960 Land Rover lilivunjwa kioo cha mlango wa
mbele kulia na basi la Kampuni ya Shabaha
lililokuwa likitokea Mwanza kwenda Dar es Salaam lilivunjwa kioo cha mbele.
Kamanda MISIME
amesema chanzo cha vurugu hizo ni wabeba mizigo wa soko la mazao kibaigwa
kupinga kitendo cha Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kuweka tangazo la kutoza
ushuru wa mazao sokoni hapo wakidai kwamba linawakosesha kufanya kazi zao kwani
wateja wanashindwa kuingiza mazao sokoni na wao kukosa kazi.
Katika hatua
nyingine Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa makosa ya kupatikana na
Mashamba ya Bangi. LEONARD S/O RAMADHANI MTWANGU, miaka 53, kabila Mgogo,
Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Ilolo Wilaya ya Mpawapwa alikamatwa akimiliki
ekari tatu (3) za shamba la bangi kinyume cha sheria. Mtu wa pili ni MATONYA
S/O MPARE mwenye miaka 24, kabila Mgogo mkazi wa Kijiji cha Matumbulu Manispaa
ya Dodoma alikamatwa akimiliki nusu ekari ya shamba la bangi kinyume cha sheria
na mtu mwingine ni EMMANUEL S/O LUHANGA mwenye miaka 45, kabila Mkaguru,
Mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Nguji Wilaya ya Kongwa ambaye alikamatwa
akimiliki ekari tatu (3) za shamba la bangi kinyume cha sheria. Watuhumiwa wote
watafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika na msako unaendelea.
No comments:
Post a Comment