Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 20, 2014

AJINYONGA KWA KUKOSA KODI YA CHUMBA


Marehemu Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika jijini Dar aliyejinyonga kwa kukosa kodi ya chumba.



Marehemu Geofrey Ndibalema (wa pili kulia) enzi za uhai wake.
INASIKITISHA! Geofrey Ndibalema (41), mkazi wa Tandika jijini Dar amedaiwa kujinyonga kwa kukosa kodi ya chumba.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea Juni 14, mwaka huu katika nyumba aliyopanga marehemu ambapo ilidaiwa kuwa siku moja kabla ya tukio, baba 

mwenye nyumba alimpigia simu kumkumbushia akaahidi kulipa siku iliyofuata ambayo ndiyo alikutwa amejinyonga.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu aliyeomba hifadhi ya jina lake, alisema Geofrey aliamka asubuhi akiwa mzima wa afya na kwenda kuchota maji ya kuoga ili aelekee kwenye shughuli zake za upambaji ambapo ilidaiwa kuwa alipewa tenda ya kupamba katika harusi na tayari alishachukua nusu ya malipo.
Ndugu huyo wa marehemu alidai, wakati Geofrey anarudi kuchota maji, alimkuta mwenye nyumba akiwa anamsubiri ili alipe kodi yake jambo lililodaiwa kumpa hofu marehemu na kuingia ndani ya chumba chake na kujinyonga.

No comments:

Post a Comment