Mkazi
wa Tandika, Protace Mungodo (60) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Ilala, kujibu mashitaka ya kujifanya profesa wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
(OUT).
Wakili wa Serikali, Gloria
Mwenda alidai mbele ya Hakimu John Msafiri kuwa Desemba 16 mwaka jana, maeneo
ya Kariakoo Wilaya ya Ilala, Mungodo alijitambulisha kwa Patrick Mavika kuwa ni
profesa wa chuo hicho.
Mshitakiwa alikana
mashitaka na alirudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana.
Alitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminiwa, watakaosaini kulipa Sh milioni
moja. Kesi itatajwa Juni 10 mwaka huu.
Wakati huo huo, Mwajuma Hamis (40)
amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Kariakoo, kujibu mashitaka ya
kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.
Karani Lucy Rutabanzibwa
alidai mbele ya Hakimu Mwajuma Diwani kuwa Februari 2 mwaka huu maeneo ya
Sokoni Manzese, alijipatia Sh 90,000 na
simu ya mkononi ambayo haikubainishwa ni
aina gani yenye thamani ya Sh 100,000 mali ya Asha Deogratius.
Mshitakiwa alikana
mashitaka na alirudishwa rumande baada ya kushindwa masharti ya dhamana,
alitakiwa kuwa na wadhamini wawili, watakaosaini kulipa Sh 200,000. Kesi
itatajwa Juni 12 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment