MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata
ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya
baada ya kuvimba mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama kipele kidogo miaka zaidi
ya 10 iliyopita lakini kadiri siku
zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa
mbavu.
Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea
nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na
homa kali hasa nyakati za usiku.
“Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida
naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata
matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko
pale pale,” alisema Nata.
Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2)
alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini
hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo
ulipofikia na kumkosesha raha.
“Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze
kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa
raha kama wengine,” alisema Nata.
Kwa upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka
mwanae kwenye hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna
mafanikio yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo
linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari naomba
wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu sahihi,” alisema
Mumbi.
Aidha alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda
hospitali mwanae anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya
kumpatia matibabu.
No comments:
Post a Comment