Brazil ilitamatisha mechi za kundi kwa kishindo iliilaza
Cameroon 4-1
Neymar alifunga mara mbili katika mechi aliyokuwa mchezaji
bora wakati Brazil ilipoishinda nguvu Cameroon na kufuzu katika raundi ya
muondoano.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 2
katika kipindi cha kwanza baada ya bao la kusawazisha lake Joel Matip, huku
Fred na Fernandinho wakihakikishia timu hiyo nafasi katika mkondo wa pili wa
timu 16 bora kama washindi wa kundi A.
Kushiriki kwa Brazil katika robo fainali kunategemea mechi
yao dhidi ya Chile katika robo fainali, na Brazil watakwenda katika mechi hiyo
itakayochezewa jijini Belo Horizonte siku ya Jumamosi wakiwa na imani mpya ya
kunyakua taji hilo.
Matokeo duni dhidi ya Croatia na Mexico yameibua wasiwasi
kuhusu Brazil - na hofu inasalia katika safu yao ya ulinzi - lakini Neymar
akiwepo, chochote chaweza kutokea.
Mshambulizi huyo wa Barcelona alirejea na bao dhidi ya Japan
katika mechi ya ufunguzi katika mechi ya kwanza ya Kombe la Mashirika la mwaka
uliopita, ambayo iliisaidia Brazil kuanza kwa ushindi ili kunyakua taji hilo,
na kocha Luiz Felipe Scolari atatumai kuwa matokeo haya yatakuwa na athari
sawa.
Scolari alitaja kikosi sawa na kile kilichoishinda Japan,
kumaanisha kuwa Hulk alirejea kutoka kwenye jeraha na kuchukua nafasi yake
Ramires katika mfumo wa 4-3-3, sawa na ulioishinda Croatia.
Brazil ilikuwa karibu kupata bao la kwanza mkwaju wake
Paulinho ulipozuiliwa baada ya Hulk kumpigia pasi iliyokuwa imetoka kwake
Neymar, lakini tamaa yao ya kushambulia ikawafanya kusahau safu ya ulinzi,
ambayo Cameroon ilonekana kutaka kutumia.
Marcelo aliokoa mkwaju ambao angefunga Vincent Aboubakar
kabla ya David Luiz kulazimika kuondoa mkwaju aliokuwa ameupiga Eric Choupo
Moting katika eneo la lango.
Hata hivyo, Brazil walionekana wasiokata tamaa, Luiz Gustavo
alipata mpira katika ubavu wa kushoto na kumpigia pasi Neymar ambaye alimpiku
Charles Itandje na kufunga bao.
Ilikuwa njia nzuri ya kuandikisha bao la 100 katika Kombe la
Dunia - na mchezaji yuyo huyo alikaribia kufunga bao la pili ambalo Itandje
aliondoa.
Uwanja uliokuwa umejaa kelele ulinyamaza kimya wakati
Cameroon walipoweka wazi safu hafifu ya ulinzi ya Brazil, Nyom akimpiku Dani
Alves na kumpigia pasi Matip aliyefunga kwa karibu.
Scolari aliwaashiria wachezaji wake, nao wakamjibu kwa njia
ya pekee wanayojua, Marcelo kumpigia Neymar pasi ambaye alikimbia na kuwapiga
chenga mabeki 2 wa Cameroon na kufunga bao lake la 35 katika mechi 52 za
kimataifa.
Scolari alimwondoa Paulinho na kumweka Fernandinho wakati wa
mapumziko .
Kiungo huyo wa Manchester City alichangia nipe nikupe
iliyozaa bao lake Fred .
Fernandinho alifunga bao la nne na kuonyesha kuwa kuwepo
kwake kulichangia ushindi huo.
No comments:
Post a Comment