Malalamiko ya wasanii kuibiana au kupigana kanzu kwenye kazi
zao yaliripotiwa sana mwaka jana na mwaka huu mambo yalikuwa shwari, lakini
baada ya kuvuka nusu ya mwaka yameibuka tena.
Mshiriki wa shindano la kuimba la Bongo Star Search (BSS) ,
Wababa amewatuhumu maswaiba wa ‘Muziki Gani’ Nay wa Mitego na Diamond Platinumz
kwa kumuibia kazi zake kwa wakati tofauti.
Akiongea kupitia Friday Night Live ya East Africa TV, Wababa
amesema Diamond amemuibia wimbo wake ambao alikua anaiita ‘Kitorondo’ na kwamba
aliibadilisha jina baadae.
“Kiukweli kuhusu Diamond, mimi mwenyewe nimetumiwa hiyo
ngoma ambayo ameitoa, nimeiskiliza jinsi ilivyo kuanzia idea, mwendo, style
ambazo anafanya. Ambayo ameibadilisha jina tu baada ya ya kwamba ilikuwa
mitandaoni nilikuwa nimemfatilia ilikuwa inaitwa Kitorondo mwezi mmoja kama
uliopita. Kwa hiyo nilishindwa kulalamika kwa sababu yeye mwenyewe alikuwa
analalamika kuwa imevuja. Kwa hiyo sikuona sababu ya kuongea kitu kwa sababu
haikuwa official. Kwa hiyo sikuwa na sababu ya kucomplaini kwa sababu haikuwa
official, lakini mpaka jana ina maana ilikuwa serious kama biashara.” Ameeleza
Wababa.
Alipoulizwa ni wapi ambapo Diamond aliusikia wimbo huo,
amesema huo ni wimbo wake alioutoa miaka minne iliyopita akiwa na Dogo Asley na
aliuweka kwenye mtandao wakati anatumia jina la Nurdi, kabla hajaanza kutumia
jina la Wababa aliposhiriki BSS. “Ni nyimbo ambayo
iko mtaani na watu wengi
wanaielewa. Kwa hiyo sijaelewa..”
Kwa upande mwingine, Wababa amedai kuwa alifanya kazi na Nay
wa Mitego katika studio za Mazoo lakini baaadae Nay alirudi studio na kuongea
na Mazoo kutaka kuunua wimbo huo kwa shilingi milioni moja bila kumshirikisha
Wababa.
“Hivi karibuni nimefanya ngoma mpya na Nay wa Mitego, ni
ngoma ambayo ilikuwa iko paid kwake pamoja na studio. Lakini kitu cha
kushangaza ni kwamba siku mbili baada ya kufanya kazi nikapigiwa simu na
producer akaniambia kwamba jamaa amerudi tena kwa ajili ya kutaka kununua wimbo
kwa milioni moja, auchukue wimbo aende akaufanye sehemu nyingine. Baada ya hapo
hata mahusiano yangu na mshikaji yamekuwa sio mazuri. Ukimpigia simu anakwambia
yuko busy kuna kazi anafanya atanicheki, hadi kufikia leo sielewi.”
Nay alipigiwa simu lakini hakuwa anapatikana kwa muda huo.
-Swahilitz
No comments:
Post a Comment