Kijana mmoja aliyejulikana kwa jina la Jumanne Joel(25-30)
ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kumvamia Monica Lutonja(32) wa kijiji cha Nyankumbu katika kata ya
Kalangalala mjini Geita .Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo
inadaiwa kuwa watu watatu akiwemo marehemu walienda kwa mama huyo na kugonga
hodi wakidai kuwa wao na rafiki wa kaka yake ambaye ni Bunegezi.Baada ya Monica
Lutonja kufungua
walianza kumkatakata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake
hadi kupoteza fahamu.Hata hivyo kelele za mama huyo zilisababisha majirani
kutoka na kuanza kuwasaka baada ya kuwa wamekimbia na hatimaye wakamkamata
mmoja na wakaanza kumpiga hadi kumuua.Kamanda wa polisi mkoa wa Geita Joseph
Konyo amethibisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa watuhumiwa wengine wawili bado wanatafutwa na
jeshi la polisi kwa ajili ya kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Na Valence Robert-Malunde1 Blog- Geita
No comments:
Post a Comment