Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, June 6, 2014

DOH WAZUNGU BWANA:::TAZAMA PICHA ZA kipindi cha TV kuonyesha Wanawake wanaojifungulia porini.




Kampuni ya Lifetime ya nchini Marekani imetangaza kipindi kipya cha Televisheni kitakachoonyesha wazazi vijana wakijifungua porini bila msaada wa madaktari wakati wa hatua zote za kujifungua lakini pia hawatakuwa na malazi yoyote katika eneo hilo.


Kipindi hicho “Born in the Wild” kitatoa taswira kwa wanawake na wanaume ambao wanaamini kuwa kujifunga mtoto katika mazingira mazuri na kupatiwa huduma zote mbali na madaktari ni njia pekee.


Kipindi hicho kimetokana na video iliyopata umaarufu mkubwa katika mtandao wa YouTube na kutazamwa mara milioni 20 ikionyesha mwanamke akijifungua porini lakini tayari wakosoaji wa mambo wanasema kipindi hicho kinaweza kutoa taswira ya kuhatarisha maisha ya wamama na watoto wanaopitia mazingira hayo.

Picha hizi zimetolewa na gazeti la Daily mail UK.

No comments:

Post a Comment