Cameroon sasa wameenda Brazil baada ya mzozo kuhusu
marupurupu yao kutatuliwa.
Wachezaji hao , almaarufu 'Indomitable Lions' walikuwa
wamesusia kuingia ndegeni hadi marupurupu yao yaongezwe.Akiwemo nyota wao
mshambuliaji wa Chelsea, Samuel Eto'o, walikuwa wamegoma kuingia ndegeni hapo
Jumapili asubuhi hivyo safari ikachelewa kwa zaidi ya saa 12.
Wachezaji hao walikuwa wakilalamikia kiwango cha fedha
£61,000 ambazo walikuwa wamepangiwa kupewa wakisema hazingetosha.
Haijabainika
vyema ni idadi gani walichoongezewa ndio wakakubali safari.Hata hivyo rais wa
shirikisho la soka la Cameroon Bw.Joseph Owona amesema 'baada ya kuweka kila
kitu wazi ,mzozo huo umetatuliwa na sasa hamna tatizo'.
Tatizo lililopo sasa kwa masimba hao ni kupata mkakati
madhubuti wa kukabiliana vilivyo na timu za kundi lao A ambamo wamo miamba ya
soka wenyeji Brazil, Croatia na Mexico.
No comments:
Post a Comment