Kaka wa marehemu (Munili Omary), Omary akiwa kwenye msiba wa
mdogo wake.
Tukio hilo lililoacha simanzi kwa wanafamilia na wakazi wa
Kitongoji cha Mpakani lilitokea saa 2 asubuhi ya Juni 18, mwaka huu.
WAKATI wanaharakati wanaendelea kupiga kelele kuhusu
kushamiri kwa vitendo vya unyanyasaji kwa watoto duniani kote, mwanamke aliyetajwa kwa jina la Amina Hamis,
mkazi wa Kata ya Kwembe, Malamba Mawili Kitongoji cha Mpakani, Kinondoni jijini
Dar ametiwa mbaroni kwa madai ya kumuua
kwa kipigo mtoto Munili Omar (6).
Awali, habari za madai ya mtoto huyo kuuawa yalitua kwenye
chumba cha habari cha Uwazi ambapo mwandishi wetu alifunga safari hadi eneo la
tukio.
Mtu wa kwanza kuonana
naye alikuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa, James Nyanda ambaye alikiri
kutokea kwa mauaji hayo ya kikatili.
Mwanamke aliyetajwa kwa jina la Amina Hamis, mkazi wa Kata
ya Kwembe, Malamba Mawili Kitongoji cha Mpakani, Kinondoni jijini Dar
anayeshikiliwa kwa kesi ya kumuua mwanaye
MAMA ADAIWA KUYUMBISHA MAELEZO
Akizungumza na gazeti hili kuhusu mkasa mzima wa mtoto huyo,
mwenyekiti huyo alisema:
“Ilikuwa saa 2 asubuhi ya Juni 19, nikiwa nyumbani kwangu
nilipigiwa simu na msamaria mwema na kunifahamisha kwamba nyumbani kwa Juma
Omar kulikuwa na msiba wa kutatanisha uliotokea jana yake, yaani Juni 18
asubuhi
Baba wa marehemu, Bw. Juma Omar.
“Baada ya kupata taarifa hiyo, saa 3 asubuhi nilikwenda eneo
la tukio na kukutana na Amina anayetuhumiwa kufanya mauaji hayo akiwa na baadhi
ya ndugu, majirani na wifi yake anaitwa Faudhia Idd. Nilihoji kuhusiana na kifo
hicho, wakaniambia mtoto alifariki dunia baada ya kuanguka.
“Niliuliza sababu ya kukaa na maiti hiyo ndani kwa siku
nzima bila kuipeleka hospitali, nikajibiwa alikuwa akimsubiri mumewe ambaye
hakuwepo.
Shangazi wa marehemu Faudhia Iddi (kulia) akiwa na
waombolezaji wengine.
“Niliomba namba za simu za mumewe ili nimjulishe msiba huo,
akanipa. Nilimpigia, nikamweleza mwanaye amefariki dunia hivyo arejee nyumbani,
akaniambia alikuwa safarini Ilula (Iringa) hivyo mtoto azikwe tu.
“Alipotoa kauli ile nilishangaa sana, nikamwambia arudi
nyumbani kwa sababu tusingeweza kumzika mwanaye bila yeye kuwepo, akasema
atarudi.”
Bibi wa marehemu (kulia) akiwa na waombolezaji wengine.
POLISI WAPIGIWA SIMU KUJULISHWA
Mwenyekiti huyo aliendelea kusema: “Kutokana na utata wa
kifo hicho niliamua kuwapigia simu polisi
wa Kituo cha Mbezi Kwayusuf ambao walifika, wakamchukua Amina, wifi yake na
mwili wa mtoto huyo wakaupelea kuuhifadhi Hospitali ya Tumbi (Kibaha) kisha
mama huyo kushikiliwa kituoni kumsubiri mumewe.
“Mume ambaye hakujua kiini cha kifo cha mwanaye alipowasili
aliunganishwa na mkewe kituoni lakini polisi walishindwa kuwa na ushahidi wa
mtoto huyo kuuawa hivyo waliandika RB ya KIFO CHA UTATA kisha wakaruhusiwa
kurudi nyumbani kuandaa taratibu za mazishi ya mtoto wao,” alisema mwenyekiti.
Waombolezaji wakiuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya
maziko.
FAUDHIA ALIFUNGUKIA UWAZI
Akizungumza na Uwazi msibani hapo, Faudhia alisema:
“Siku ya tukio ambayo ilikuwa Juni 18, Munila alikojoa
kitandani ndipo wifi alimtoa sebuleni na kuanza kumchapa kwa kutumia mkanda.
Alipoona mtoto ametulia, aliniita na kuniambia Munili alianguka hivyo niende
nikamwite nesi anayemiliki duka la dawa mtaani, nilimwona Munili akitokwa povu
mdomoni, jeraha la kupigwa na mkanda kwenye paji la uso na shingoni,
nilipomuuliza alipatwa na nini akaniambia alianguka.
“Nilipofika kwa nesi akaniambia kama mtoto alizidiwa
tumpeleke hospitali, nilirudi nyumbani na kumweleza wifi, ndipo akachukua maji
ya baridi na kummwagia Munili lakini hakuamka, alichukua kitenge akampepea
lakini Munili alitulia kimya.
Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Mpakani wakiwa wameubeba
mwili wa marehemu Munili.
“Wifi akanituma niende kumwita mama Aneth ambaye ni jirani, alipofika alimwangalia
mtoto akashauri akaitwe mjumbe ambaye hakuwepo. Nikamfuata Shehe Mpitanga
ambaye alipofika na kumwangalia mtoto akasema alishafariki dunia, wifi akaanza
kulia.”
Faudhia aliongeza kuwa, alipowaeleza ukweli akina mama
kuhusiana na tukio hilo, wifi yake alitoka ndani na kutaka kutoroka lakini
walifanikiwa kumnasa ndipo nilichukuliwa mimi, kaka (baba wa marehemu), tukapelekwa
tena polisi ambako nilieleza kilichotokea, wakaamua kuwashikilia wao hadi leo
(Juni 21, mwaka huu).
KAMANDA WA POLISI AZUNGUMZA
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camilius Wambura
alipopigiwa simu na kuulizwa kama alikuwa na taarifa ya mauaji hayo alisema
hakuwa na taarifa ila atafuatilia.
No comments:
Post a Comment