MWILI wa Idd Shamba aliyefariki dunia kwa ajali ya
barabarabi katika Kijiji cha Engaruka wilayani hapa, imekaa barabarani kwa
zaidi ya saa 21 ikisubiri polisi na daktari kufika eneo la tukio kwa ajli ya
kupima ajali hiyo na kuufanyia uchunguzi mwili huo kabla kwenda kuzikwa.Polisi
walifika eneo la tukio majira ya saa saba mchana ikiwa ni saa 18 tangu kutokea
kwa ajali hiyo ambapo baada ya kumaliza kazi ya kukagua na kupima eneo la
ajali, mwili huo ulihamishiwa chini ya mti kuukinga na jua usiharibike wakati
wakisubiri daktari kuja kuufanyia uchunguzi.Tanzania Daima ilishuhudia wananchi
na viongozi wa Kata ya Engaruka wakiulinda mwili huo wakati akisubiriwa daktari
kutoka Mto wa Mbu ambaye naye alifika eneo la tukio majira ya saa 10
jioni.Ajali hiyo ilitokea Juni 12 mwaka huu baada ya Shamba kudondoka kutoka
kwenye gari la mizigo aina ya Toyota DCM, lenye namba za usajili T 995 AMB
lililokuwa likitokea mnadani Engaruka kwenda Kijiji cha Selela.
Diwani wa kata hiyo, Pashet Sengerwan (CCM), alisema kuwa
mwili huo ulifanyiwa uchunguzi kwenye eneo la ajali kisha kuzikwa Juni 13,
majira ya saa 11 jioni kwenye makaburi ya kijijini hapo bila kuwasubiri ndugu
zake waliokuwa wakitokea Singida.Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Liberatus
Sabas, alisema tayari wameshamhoji mmiliki wa gari hilo, Sauli Kitomari huku
wakiendelea na juhudi za kumtafuta dereva wa gari hilo ambaye alitoroka mara
baada ya kutokea ajali hiyo.
Alisema kuchelewa kwa polisi kufika eneo la tukio,
kulitokana na kukosekana kwa kituo cha polisi kwenye eneo la Engaruka ambalo
pia lina tatizo la mawasiliano ya simu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Moduli, Dowika Kasunga,
alisema hali hiyo ilisababishwa na tatizo la mawasiliano na mamlaka husika
kwani katika Kata ya Engaruka ili upige simu, lazima uende umbali mrefu
kutafuta mawasiliano hayo.
No comments:
Post a Comment