Waziri wa sheria Mark Golding, amesema kuwa baraza la
mawaziri linaunga mkono pendekezo kuwa kiwango kidogo zaidi cha Bangi,
kitakachoruhusiwa kwa mtu kumiliki kitakuwa gramu 57.
Bwana Golding amesema kuwa Marijuana itaweza kuhalalishwa
kwa kiwango kidogo kwa sababu za kidini , matibabu na utafiti wa kisayansi.
Inatarajiwa kuwa bunge la nchi hjiyo litaweza kupitisha
mswada huo ifikapo mwezi Septemba.
"nataka nisisitize kuwa magezi yanayopendekezwa
kufanyiwa sheria hayalengi kuhalalisha matumizi ya Bhangi kwa sababu ya
kujiburudisha,'' alisema bwana Golding.
Lengo ni kuwezesha muelekeo mzuri wa kukabiliana na visa vya
watu wanaopatikana wakiwa na viwango vidogo vya Bangi.
Wandishi wa habari wanasema mipango ya serikali ni kama
ushindi kwa watu wa Rastafaria ambao wanaamini kuwa Ganja ni kitu kitakatifu.
Mageuzi ya hivi karibuni katika nchi kama vile Uruguay au
majimbo kadhaa nchini Marekani, kama vile Colorado, yameweza kushinikiza zaidi
kampeini ya wakulima wa Bangi pamoja na sheria kuhalalisha matumizi ya mmea
huo.
"sio jambo zuri kuendelea kudhibiti matumizi ya Bangi
au kuendelea kusisitiza sheria inayowazuia watu kumiliki Ganja kwa sababu za
kimatibabu,'' asema bwana Golding
Bi Angela Brown Burke, meya wa mji Kingston, alinukuliwa
akisema : "muda umewadia kutoa fursa kwa wajamaica kunufaika kutokana na
biashara za Marijuana.
No comments:
Post a Comment