Serikali ya Uganda imekipiga marufuku kituo cha runinga cha
NTV kufanya habari yoyote inayohusu ikulu au rais wa Uganda baada ya kuonesha
picha ya rais Yoweri Kaguta Museveni akiwa amelala bungeni.
Meneja wa masuala ya vyombo vya habari wa serikali ya
Uganda, Dennis Katungi aliiambia AFP sababu za kuifungia NTV kuonesha habari za
ikulu/rais.
“Wao wanafahamu kabisa kuwa rais huwa anatabia ya
ku-meditate halafu bado wanaenda nje wanasema alikuwa amelala.” Alisema
Katungi.
Nae msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo
alithibitisha hatua iliyochukuliwa dhidi
ya NTV Uganda ambayo ni sehemu ya
National Media Group .
“Tumewasimisha kutotoa habari zote zinazomhusu rais kwa
kuzingatia uhusiano wetu na wao.” Amesema Ofwono na kukituhumu kituo hicho kwa
upungufu wa weledi na kuegemea upande mmoja.
Hata hivyo alisisitiza kuwa wamesimamishwa kwa muda na sio
moja kwa moja.
Rais Museveni ana umri wa miaka 69 hivi sasa.
Serikali ya Uganda imekipiga marufuku kituo cha runinga cha
NTV kufanya habari yoyote inayohusu ikulu au rais wa Uganda baada ya kuonesha
picha ya rais Yoweri Kaguta Museveni akiwa amelala bungeni.
Meneja wa masuala ya vyombo vya habari wa serikali ya
Uganda, Dennis Katungi aliiambia AFP sababu za kuifungia NTV kuonesha habari za
ikul/rais.
“Wao wanafahamu kabisa kuwa rais huwa anatabia ya
ku-meditate halafu bado wanaenda nje wanasema alikuwa amelala.” Alisema
Katungi.
Nae msemaji wa serikali ya Uganda, Ofwono Opondo
alithibitisha hatua iliyochukuliwa dhidi ya NTV Uganda ambayo ni sehemu ya
National Media Group .
“Tumewasimisha kutotoa habari zote zinazomhusu rais kwa
kuzingatia uhusiano wetu na wao.” Amesema Ofwono na kukituhumu kituo hicho kwa
upungufu wa weledi na kuegemea upande mmoja.
Hata hivyo alisisitiza kuwa wamesimamishwa kwa muda na sio
moja kwa moja.
Rais Museveni ana umri wa miaka 69 hivi sasa.
No comments:
Post a Comment