Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, June 4, 2014

MAJINA YA KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA BOSNIA KWA AJILI YA KOMBE LA DUNIA


Bosnia-Herzegovina imethibitisha kikosi chake kwa ajili ya kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil.

Ervin Zukanovic ameondolewa katika kikosi hicho baada ya kushindwa kusafiri na timu kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kambi kutokana na kukosa Visa.

Beki huyo wa Gent alikaririwa akililalamikia shirikisho la Bosnia kwa tukio hilo, lakini viongozi walithibitisha kuwa mchezaji huyo hatakiwi tena Brazil.


Kocha wa Bosnia, Safet Susic awali alitaja kikosi cha wachezaji 24, hivyo kukosekana kwa Zukanovic kunamaanisha wachezaji wengine wote waliocgaguliwa awali wataenda Brazil.

Bosnia watacheza na Mexico katika mechi ya mwisho ya kujipima ubavu kesho jumatano, kabla ya kuvaana na Argentina, Nigeria na Iran kwenye Kundi F kombe la dunia.

Kikosi Kizima hiki hapa:

Walinda Mlango: Asmir Avdukic (Borac Banja Luka), Asmir Begovic (Stoke City), Jasmin Fezjic (Aalen).

Mabeki: Muhamed Besic (Ferencvaros), Ermin Bicakcic (Eintracht Braunschweig), Sead Kolasinac (Schalke), Emir Spahic (Bayer Leverkusen), Toni Sunjic (Zorya), Ognjen Vranjes (Elazigspor).

Viungo: Anel Hadzic (Sturm Graz), Izet Hajrovic (Galatasaray), Senijad Ibricic (Erciyespor), Senad Lulic (Lazio), Haris Medunjanin (Gaziantepspor), Zvjezdan Misimovic (Guizhou Renhe), Mensur Mujdza (Freiburg), Miralem Pjanic (Roma), Sejad Salihovic (Hoffenheim), Tino Susic (Hajduk Split), Edin Visca (Istanbul BB), Avdija Vrsajevic (Hajduk Split).

Washambuliaji: Edin Dzeko (Manchester City), Vedad Ibisevic (Stuttgart).

No comments:

Post a Comment