Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao (kushoto) akiangalia ramani ambayo reli ya TAZARA inapita kuanzia kituo cha Dar es Salaam wakati alipotembelea Makao Makuu ya Shirika la Reli la Tanzania na Zambia (TAZARA) leo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuangalia miundo mbinu ikiwemo mabehewa na injini za treni za shirika hilo. Kulia ni Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe.
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe akishuka toka ndani ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Li Yuanchao akishuka toka ndani ya treni ya abiria ya TAZARA kuelekea katika kituo cha mizigo cha TAZARA kilichopo mtaa wa Yombo jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupatiwa maelezo ya kina kuhusiana na reli hiyo.
PICHA ZOTE NA BENEDICT LIWENGA-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment