Ndugu zangu,
Ujangili umeendelea kushika kasi nchini Tanzania, hasa wa
tembo, licha ya jitihada kadhaa zinazofanywa na mamlaka husika.Tembo kama huyu
pichani anauawa kinyama na wendawazimu wachache ambao wanaangalia maslahi yao
ya kuuza meno yake bila kujali hatma ya baadaye ya rasilimali zetu.
Zimekuwepo operesheni nyingi nchini, miongoni mwazo ni ile
ya Tokomeza Ujangili iliyoendeshwa mwaka 2013, ambayo ilisitishwa baada ya
kudaiwa kwamba wasimamizi wake waliendesha vitendo vya utesaji kwa wale
walioshukiwa kujihusisha na ujangili.Lakini pamoja na kusitishwa huko, bado
kikwazo kikubwa kinaonekana kipo serikalini, kwani tunaelezwa kwamba wapo
maofisa wakubwa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu, na wanatengeneza
mamilioni ya fedha.
Ndugu zangu, lazima tuwe wazalendo, tuungane kwa pamoja
kupinga unyama na ujambazi huu ambao kama hatukisimama imara unaweza
kuwapukutisha hayawani wote nchini na tukabaki na picha za wanyama kwenye
vitabu vyetu vya historia. Tembo ndiye mnyama mkubwa kabisa aliyesalia duniani
katika jamii zile za dinosaur, hivyo ni urithi mwingine kwa vizazi vyetu.
Ndugu yenu,
Daniel Mbega,Iringa – Tanzania


No comments:
Post a Comment