Andrey Coutinho akisaini mkataba wa kuitumikia Yanga kwa
kipindi cha miaka miwili mbele ya Katibu Mkuu Beno Njovu leo makao makuu ya
klabu
Kiungo mshamabuliaji Andrey Marcel Ferreira Coutinho raia wa
Brazil leo amesaini mkataba wa miwili kuitumikia timu ya Young Africans kwa
ajili ya michuano mbalimbali ikiwemo ya Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na
mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katibu mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema usajliwa mchezaji
Coutinho ni sehem ya muendelezo wa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na kama
ilivyokawaida wao mambo yao ni kimyakimya.
Coutinho ambaye alizaliwa tarehe 12 Januari 1990 amekulia
kwenye mji wa Berem ambapo alianza kucheza soka la kulipwa katika klabu ya
Paysandu Sports Club kabla ya kwenda nchini Asia katika nchi ya Myanmar katika
klabu ya Rukhapura United.
Mpaka anajiunga na klabu ya Young Africans Andrey Coutinho
alikuwa akichezea timu ya Castanhal EC iliyopo kwenye Ligi Daraja la pili ambao
aliweza kuichezea kwa michezo yote ya
mzunguko wa pili mwaka 2014.
Katika hatua nyingine kikosi cha Young Africans kinatarajia
kuendelea na mazoezi kesho chini ya kocha Marcio Maximo katika ufuke wa Coco
Beach ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi baada ya leo kuwa na mkutano wa
ndani na wachezaji wake pamoja na benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment