Mtawa wa Italia anyakua ushindi
Mtawa mmoja kutoka Italia ambaye alipata umaarufu katika
mtandao wa kijamii ameshinda shindano la kuimba nchini humo.Mtawa huyo, Sister
Christina Scuccia alitokea kwa mara ya kwanza katika televisheni kushiriki
shindano la The Voice.Scuccia aliyeonekana amevalia mavazi yake ya utawa na
msalaba shingoni, alijawa na furaha na kumshukuru Mungu kwa kumfikisha katika
ushindi huo.
Mtindo wake wa wimbo wa Alicia Keys, kwa jina 'No One',
umetizamwa zaidi ya mara milioni 50 katika mtandao wa You Tube tangu auimbe.Mtawa
huyo mwenye umri wa miaka 25 amesema kuwa aliamua kushiriki mashindano hayo
kufuata ushauri wa Papa mtakatifu Francis, kuwa kanisa liwakaribie zaidi watu
wa kawaida.Chanzo BBC
No comments:
Post a Comment