Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 2, 2014

MTOTO WA BOKSI MAREHEMU "NASRA MVUNGI" KUAGWA UWANJA WA JAMHURI MOROGORO


Uwanja wa JAMHURI mkoani Morogoro utatumika kumuaga mtoto Nasra Mvungi aliyefariki jana alfajiri  hospitali ya Muhimbili.



Hayo yamesemwa na Ofisa ustawi wa jamii mkoani Morogoro, Oswin Ngungamtitu.



Amesema idara hiyo kwa kushirikiana na jeshi la Polisi   imepanga kusimamia mazishi ya mtoto Nasra Mvungi (4) maarufu katika magazeti kama mtoto wa boksi.



Mtoto huyo alifariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili alikokuwa amelazwa kutokana na magonjwa mbalimbali yanayosadikiwa kusababishwa kwake ndani ya boksi kwa zaidi ya miaka  mitatu.




Aidha kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro John Laswai alisema kuwa baada ya kifo cha mtoto

huyo taratibu za kipolisi zitafanywa ikiwa ni pamoja na kupata taarifa ya daktari ambayo itaeleza sababu za kifo cha mtoto huyo.



Alisema kuwa taarifa hiyo ikishatolewa itapelekwa kwa wanasheria ambaye ataipitia na kuangalia sheria inavyosema na kama taarifa hiyo itaeleza sababu za kifo kuwa imetokana na ukatili na watuhumiwa hao basi watakamatwa na kesi itabadilika.

No comments:

Post a Comment