Polisi Kaskazini mashariki mwa Nigeria wanasema kuwa
shambulizi la bomu limewauwa zaidi ya watu 14 na kuwajeruhi wengine wengi.
Ripoti zimesema kuwa mlipuko huo uliotokea katika mji wa
Mubi, ulilenga chumba kimoja cha burudani ambako watu walikuwa wakitazama mechi
ya soka kwenye televisheni.Katika miezi michache iliyopita, Boko Haram
wamezidisha mashambulio yao hasa kaskazini mashariki mwa Nigeria. Mamia ya watu
wameuawa na wengine wengi kujieruhiwa.Pia wameshambulia nyumba za watu na
kuzichoma moto, na kisa kilicho tikisa jamii ya kimataifa ni wasichana zaidi ya
200 waliotekwa nyara yapata miezi miwili sasa hadi leo hawajulikani waliko.
'Uharibifu uliozidi'
Mashambulio haya yameacha uharibifu mkubwa. Waliosalimika
wamelazimika kukimbia makwao huku shule zikiachwa bila wanafunzi.Shambulio hilo
limetokea karibu na mpaka kati ya Nigeria na Cameroon katika jimbo la
Adamawa-mojawepo ya majimbo ambako sheria ya hali ya hatari inatumika kutokana
na mashambulizi ya kundi la waislamu wenye itikadi kali la Boko Haramu.Katika
mwezi mmoja pekee watu zaidi ya 200 wameuawa katika mji huo.Lakini sasa katika
maeneo mengine ya kaskazini ambako inasemekana usalama umerejea kiasi, kama
vile mji wa Kano juhudi zinafanywa kung'oa mizizi ya uovu huo.Wanamgambo wa
kiislamu AL shabaab wanaodaiwa kuwa na uhusiano na AL qaeda wamekuwa wakiwazuia
wananchi kushiriki mambo yanayohusishwa na Mataifa ya magharibi. Inakisiwa kuwa
zaidi ya wanafunzi milioni 11 kaskazini mwa Nigeria hawapewi mafunzo mengine
yoyote mbali na ya kidini.
'Wanafunzi waathirika'
shule za Nigeria
Mashirika ya kijamii hasa kutoka
Uingereza yamekuwa yakifadhili kupitia taasisi za nchini humo masomo ya ziada
hasa katika shule za mafunzo ya kidini, ili yatoe elimu ya ziada mbali na
Qurani.
Tayari maelfu ya wanafunzi wanafaidi
lakini bado kuna wengi zaidi wanaotishiwa usalama wao na inadaiwa ni kiasi
kikubwa zaidi ya nchi hiyo haiwezi kufikiwa.
Licha ya mauaji ya miaka mingi
yaliyofanywa na kundi hilo la Boko Haram na hata kujitangaza hadharani uhusiano
wao na kundi la AL Qaeda, ni wiki iliyopita tu ambapo Umoja wa Mataiifa
umeilitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Japo wengi wanaona kuwa hatua hiyo
imechelewa, bado inatoa matumaini ya kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kusaidia
kukabiliana na kundi hilo.
'Wanafunzi waathirika'
shule za Nigeria
Mashirika ya kijamii hasa kutoka Uingereza yamekuwa
yakifadhili kupitia taasisi za nchini humo masomo ya ziada hasa katika shule za
mafunzo ya kidini, ili yatoe elimu ya ziada mbali na Qurani.
Tayari maelfu ya wanafunzi wanafaidi lakini bado kuna wengi
zaidi wanaotishiwa usalama wao na inadaiwa ni kiasi kikubwa zaidi ya nchi hiyo
haiwezi kufikiwa.
Licha ya mauaji ya miaka mingi yaliyofanywa na kundi hilo la
Boko Haram na hata kujitangaza hadharani uhusiano wao na kundi la AL Qaeda, ni
wiki iliyopita tu ambapo Umoja wa Mataiifa umeilitangaza kuwa kundi la kigaidi.
Japo wengi wanaona kuwa hatua hiyo imechelewa, bado inatoa
matumaini ya kuweza kuchukuliwa hatua zaidi kusaidia kukabiliana na kundi hilo.
No comments:
Post a Comment