Askari polisi wa kituo kikuu cha Polisi cha kati akiwa amemshikilia kijana mmoja baada ya kumuokoa toka mikononi mwa madereva bodaboda ambao walikwishaanza kujichukulia sheria mkononi kwa kumuadhibu baada ya kutaka kuiba pikipiki.
Askari katika ofisi ya kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro walilazimika kufunga geti kuzuia kundi kubwa la madereva boda boda na watu wengine wakilazimisha kuingia ili kumfuata mwizi wao wa pikipiki. Madereva hao walionekana kukerwa na kuzuiwa kumuadhibu kijana huyo na hapa walionekana wakilalamika. Jamaa wa nje akatamani kupita katikati ya Nondo hapa.
Geti likafungwa na hakuna mtu aliyepita.
Geti likafungwa na hakuna mtu aliyepita.
No comments:
Post a Comment