Mshambuliaji wa Nigeria Peter Odemwingie (kushoto) akifunga bao lake, huku kipa Asmir Begovic akiwa hana la kufanya.
BAO pekee la mshambuliaji wa Stoke City, Peter Odemwingie katika mchezo wa kombe la dunia limeipa ushindi muhimu timu ya taifa ya Nigeria dhidi ya Bosnia.
Kwa matokeo hayo, Bosnia wameshaaga mashindano yao ya mara ya kwanza ya kombe la dunia
Kitu kambani: Odemwingie akiwa ametumbukiza mpira nyavuni.
Odemwingie (kushoto) akishangilia bao lake baada ya kupokea pasi kutoka kwa Emmanuel Emenike (kulia).
Odemwingie akipongezwa na wachezaji wenzake.
Hapa chini ni vikosi vya timu zote na viwango vyao. Alama zilizotolewa ni chini ya 10.
Kikosi cha Nigeria: Enyeama 7, Oshaniwa 6, Yobo 6, Omeruo 6, Ambrose 6, Onazi 7, Mikel 6, Babatunde 6 (Uzoenyi 75), Musa 7 (Ambeobi 66 5) Odemwingie 8, Emenike 7
Wachezaji wa akiba ambao hawakucheza: Ejide, Uzoenyi, Gabriel, Egwuekwe, Moses, Odunlami, Azeez, Nwofor, Uchebo, Agbim.
Kadi ya njano: Mikel
Mfungaji wa goli: Odemwingie
Kikosi cha Bosnia-Herzegovina: Begovic 7, Mundza 6, Sunjic 6, Spahic 5, Lulic 6 (Salihovic 58 6), Besic 7, Misimovic 6, Medunjanin 6 (Susic 64 5), Hajrovic 6 (Ibisevic 57 6), Pjanic 8, Dzeko 6
Subs not used: Fejzic, Vrsajevic, Bicakcic, Kolasinac, Vranjes, Ibricic, Visca, Hadzic, Avdukic.
Kadi ya njano: Medunjanin
Mwamuzi: Peter O'Leary (New Zealand)
*Viwango vya wachezaji na Joe Bernstein
Hakuna njia: Mshambuliaji wa Bosnia, Edin Dzeko (kulia) akiangushwa chini na kiungo wa Nigeria John Obi Mikel
Rudi hapa wewe!: mchezaji wa Bosnia, Muhamed Besic (kulia) akivuta kiatu cha Michael Babatunde baada ya kuzidiwa maarifa.
No comments:
Post a Comment