Pembe 228 za ndovu zanaswa Mombasa
Serikali ya Kenya imenasa shehena kubwa zaidi ya pembe za
ndovu 228 katika kisiwa cha Mombasa mwaka huu.Shehena hiyo ya pembe za ndovu
114 ilipatikana katika bohari moja inayotumika na kampuni ya uchukuzi.
Mshukiwa mmoja alikamatwa katika tukio hilo.
Kupatikana kwa shehena hiyo kubwa ya meno ya ndovu inatilia
pondo dhana inayotokana na utafiti wa mashirika yanayopigania kusitishwa uuzaji
wa pembe za ndovu kuwa bandari za Mombasa Kenya Togo na Dar SalaamTanzania
zinatumika kusafirisha pembe za ndovu kutoka kote barani Afrika kuelekea bara
Asia.Utashi wa pembe za ndovu na bidhaa zitokanazo na pembe nchini China na
mataifa ya Mashariki ya mbali ndio unaochochea mauaji ya tembo katika mbuga na
hifadhi mbalimbali barani Afrika.
Maafisa wadai pembe hizo zilikuwa njiani kuelekea Asia
Mbali na kuwa bidhaa ya thamani kubwa huko Asia na China
pembe za ndovu hutumika kama dawa ya kienyeji .
Shehena hii ni kubwa zaidi kuwahi kukamatwa mwaka huu
bandarini kulingana na afisa wa Huduma kwa wanyama pori nchi Kenya yaani (KWS)
Paul Muya.Afisa wa KWS alidokeza kuwa kuwa shehena hiyo kubwa ya ndovu ilitoka
katika moja ya mataifa mbalimbali yanayotumia bandari ya Mombasa kusafirisha
bidhaa zao kuelekea ughaibuni.Mwezi Aprili,Serikali ya Kenya iliwasimamisha
kazi kwa muda maafisa wakuu wa shirika la huduma kwa wanyama pori KWS kwa kile
ilichotaja kuwa ni utepetevu kazini.
Serikali Kenya wakati huo ilisema kuwa itachukua mstari wa
mbele kulinda wanyama pori.Kulingana na takwimu nchini Kenya vifaru 18 na ndovu
50 wameuawa mwaka huu idadi sawa na ile iliyosajiliwa mwaka uliopita.Wanaharaki
wa kulinda wanyama pori wanadai kuwa idadi hiyo ni chini mno kwani visa vingi
haviripotiwi.CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment