Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitalini kwa
uchunguzi wa kiafya .
Taarifa hii ni kwa mujibu wa maafisa kutoka kwa ofisi yake.
Taarifa hiyo ilisema kuwa Zuma atalazimika kumpumzika kwa muda ingawa
ataendelea na majukumu yake ya kitaifa akiwa nyumbani.
“Hapo jana Ijumaa Rais Zuma alishauriwa kupumzika hasa baada
ya msimu wa uchaguzi kukamilika wiki chache zilizopita.
Madaktari hawajaeleza
wasiwasi wowote kuhusu afya yake.’’Bwana Zuma ambaye alihusika na harakati
dhidi ya utawala wa kibaguzi, ana umri wa miaka 72 na aliapishwa kwa muhula wa
pili baada ya uchaguzi mkuu tarehe 24 mwezi Mei, ambapo chama chake ANC
kilishinda uchaguzi huo.
Baraza lake la mawaziri, lina kibarua kigumu kukabiliana na
uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kudorora kila kukicha pamoja na ukosefu wa
ajira.
Wadadisi wanasema asilimia 25 ya wananchi hawana ajira.


No comments:
Post a Comment