Ruby DEE, mmoja wa
waigizaji wa muda mrefu mjini Hollywood na Broadway alipatwa na mauti
siku ya jumatano usiku tarehe 11 akiwa na umri wa miaka 91. Ruby alikuwa
nyumbani kwake “New Rochelle, NY” … akizungukwa na familia yake wakati
mauti yanamkumba kulingana na ripoti familia yake. Ruby alikuwa pioneer
kwa “African-American Women” mjini Hollywood na alijipatia umaarufu
mkubwa kwenye filamu aliyoifanya miaka ya 1960 “A Raisin in the Sun” na
filamu ya Director Spike Lee “Do the Right Thing” na “Jungle Fever.” na
vile vile Filamu iliyochukua budget kubwa ya Hollywood ni “American
Gangster” ambayo aliigiza kama mama yake ‘Denzel Washington’.
Ruby alikuwa mshairi na screenwriter ambae alishawahi kujishindia
Grammy Awards na Emmy Awards na kupokea National Medal of Arts na
Kennedy Center Honors. Marehemu RUBY DEE na mumewe ambaye nae ni
marehemu kwa sasa Ossie Davis ambao walikuwa pia wagombea uhuru wa
weusi huko nchini Marekani wakiwa pamoja na mwanaharakati ‘Martin Luther
King Jr’ na ‘Malcolm X’. R.I.P
No comments:
Post a Comment