Na Ismail Ngayonga, MAELEZO
SERIKALI ya Jamhuri ya Watu imeikabidhi Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) msaada wa gari la kurushia Matangazo lenye thamani ya
Tsh. Bilioni 6 ili kuboresha utendaji wa shughuli za shirika hilo.
Akipokea msaada huo kwa niaba ya Serikali ya Tanzania,
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema
msaada ni kielelezo cha urafiki wa kweli wa kimaendeleo katika nyanja
mbalimbali uliopo baina ya Tanzania na China.
Mukangara alisema gari hilo litaisaidia TBC kuteleza
majukumu yake kikamilifu na hasa katika kipindi hiki ambacho matangazo mengi ya
Televisheni yamekuwa yakirushwa katika mgumo wa dijitali. “Tupo katika mradi
kwa kushirikiana na STARTIMES kuhakikisha kuwa TBC inafika katika kona zote za
Tanzania na kuwafikia wananchi kwa urahisi zaidi” alisema Waziri Mukangara.
Kwa mujibu wa Waziri Mukangara alisema Mwezi Oktoba mwaka
huu (2014) Rais Jakaya Kikwete atafanya ziara ya kikazi nchini China ambapo
pamoja na mambo mengine, Serikali ya China imepanga kuipatia Tanzania mkopo wa
liba nafuu ambao utasaidia TBC kujipanga na kufikia malengo yake kwa muda
mfupi.
Aidha Waziri Mukangara alisema upo umuhimu mkubwa wa
kuimarisha uhusiano wa vyombo vya habari baina ya Tanzania na China kwani
kutasaidia kubadilishana utamaduni baina ya nchi hizo mbili. “Kupitia Matangazo
ya televisheni tutaweza kubadilisha fikra za jamii zetu na TBC ni lazima iweze
kuwa imara katika Nyanja zote” alisema Waziri Mukangara.
Kwa upande wake Mkurungezi Mkuu wa TBC, Clement Mshana
alisema msaada huo umekuja katika wakati mwafaka kwani lengo la TBC kwa sasa
imejipanga kikamilifu sekta ya michezo
ikiwemo mpango wa kuonyesha matangazo ya moja kwa moja kutoka katika uwanja wa
Taifa Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuonyesha ulimwengu vipaji vya
wanamichezo vilivyopo Tanzania wachezaji waliopo Tanzania.
“Uwanja wa Taifa kwa sasa umekamilifu kwa kiasi kikubwa na
hasa katika eneo la mchezo wa mpira wa Miguu, na sisi tumejipanga kuonyesha
michezo yote ya mpira wa miguu kuanzia mechi za ndani hadi nje ya nchi’ alisema
Mshana.
No comments:
Post a Comment