Baada ya mvua kubwa iliyonyesha Recife na kusababisha
mafuriko kutishia kuahirishwa kwa mechi baina ya Ujerumani na Marekani,
hatimaye hali ya anga ilikuwa murwa kwa mechi hiyo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu
haswa kwa Marekani ambao walikuwa wanahitaji sare ya aina yeyote na kuomba kuwa
Black stars ya Ghana wanakunguwaa iliwao waweze kusonga mbele ktika kundi G.
Na baada ya mbivu na mbichi kubainika Ujerumani na Marekani
zote zilijikatia tikiti ya kushiriki mechi za raundi ya pili licha ya Ujerumani
kushinda mechi hiyo kwa bao moja bila ya jibu.
Bao la pekee lilifungwa na Thomas Muller
Ujerumani na Marekani zafuzu kwa raundi ya pili
Mshambulizi huyo wa Bayern Munich aliifungia Ujerumani bao
lake la 9 katika mechi sawa na hizo .
Fauka ya mvua kubwa iliyonyesha mapema taswira katika uwanja
wa Arena Pernambuco ulioko Recife ilikuwa n ushindani mkubwa baina ya Marekani
na Ujerumani.
Kufuatia matokeo hayo Marekani sasa watakwenda el Salvador
ilikuchuana na Ubeljiji jumanne ijayo katika mechi yao ya kundi la pili huku
Washindi wa kundi hilo Ujerumani wakiratibiwa kumaliza udhia dhidi ya mshindi
wa pili katika kundi H yaani ( Algeria ama Urusi)
No comments:
Post a Comment