Uvitaji wa Shisha ni sawa na uvutaji wa sigara kulingana na
madaktari
Serikali ya Tanzania imepiga marufuku uvutaji wa Shisha.
Uraibu huo unaohusisha uvutaji wa Tumbaku yenye ladha
tofauti tofauti ambayo hutiwa ndani ya chupa kubwa na kuvutwa kwa mirija,
umeshika kasi sana Tanzania hasa miongoni mwa vijana wadogo mjini Dar Es
Salaam.
Baadhi ya watu wanaiona Shisha kama isiyokuwa na madhara ya
kiafya ikilinganishwa na uvutaji wa Sigara.Lakini wataalamu wanaamini kuwa
uvutaji wa Shisha kwa muda wa saa moja ni sawa na kuvuta sigara miamoja.Madaktari
walitoa onyo kuhusu uvutaji wa Shisha wanakabiliwa na tisho la kuugua Saratani
sawa na hatari inayowakabili wavitaji wa sigara
No comments:
Post a Comment