Mwanamke mmoja mkazi
wa Kintinku, Wilayani Manyoni
mkoani Singida amejikuta
akimwaga machozi baada
ya kujifungua mtoto
mwenye kichwa cha
ajabu ( tepe tepe). Tukio hilo
limetokea jana asubuhi
katika hospitali ya
Kintinku Health Center
iliyopo Wilayani Manyoni…..
Akiongea na Mpekuzi
kwa sharti la kutotajwa jina
lake kwa madai
kuwa yeye si
msemaji wa hospitali
hiyo, Mkunga mmoja wa
hospitali hiyo amedai
kuwa mama huyo
alifikishwa hospitalini hapo
akiwa katika hatua
za mwisho kujifungua.“Alifikishwa hapa
akiwa katika hatua
za mwisho . Hakuwa
na kadi yoyote
ya Clinic kwa
kuwa hakuwahi kuhudhuria
Clinic tangu abebe
mimba hiyo.
“Pamoja na kutokuwa
na kadi ya
Clinic, tulianza kumsaidia kujifungua, lakini mtoto
aliyezaliwa alikuwa ni
wa tofauti kidogo
na alikuwa amefariki
dunia.Kichwa chake kilikuwa
tepetepe na kimebonyea bonyea.
“Ilikuwa ni ngumu
kwetu kutambua tatizo
alilokuwa nalo mama
huyo kwa kuwa
hakuwa na kadi
yoyote ya Clinic
ambayo ingeweza kutusaidia kujua
maendeleo ya mtoto
huyo alipokuwa tumboni “, alisema Mkunga
huyo.
Mpekuzi ilifanya mahojiano
na mama huyo
ambaye naye alionyesha
kushangazwa na tukio
hilo na kusema
hajui tatizo lililomfanya
ajifungue mtoto huyo
kwa kuwa hakuwahi
kusikia maumivu ya
aina yoyote wakati
wa ujauzito huo
hadi alipofikia hatua
ya kujifungua….
Katika mahojiano hayo, mama
huyo alisema kuwa
huo ni uzao
wake wa 6
na hajawahi hudhuria
Clinic
No comments:
Post a Comment