Mkongwe wa Italia, Andrea Pirlo (kushoto) akibadilishana jezi na Edisnon Cavani wa Uruguay baada ya mechi.
ITALIA imeaga Kombe la Dunia nchini Brazil baada ya kufungwa 1-0 na Uruguay, bao pekee la Diego Godin katika mchezo ambao mshambuliaji Luis Suarez alimng’ata Giorgio Chiellini.
Godin alifunga bao hilo dakika ya 81 na kipa Buffon wa Italia alilazimika kuingia uwanjani dakika ya mwisho kusaidia nguvu ya kusaka bao, Azzuri ikihtaji sare tu kusonga mbele.
Italia ilimpoteza mchezaji wake Marchisio aliyetolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Arevalo Rios dakika ya 60.
Katika mechi nyinine,Costa Rica imemaliza kileleni mwa Kundi D baada ya sare ya 0-0 na England leo ikifikisha pointi saba, Uruguay pointi sita na Italia pointi tatu, wakati England imeondoka na pointi moja.
No comments:
Post a Comment