SHIRIKA la Umeme nchini Tanesco, limesema kuwa kuzimika
ghafla kwa umeme karibu mikoa yote nchini, kumetokana na hitilafu iliyojitokeza
katika gridi ya Taifa ambayo hadi sasa haijafahamika chanzo chake, na kulilazimu
Shirika hilo kuwasha mitambo yake mingine ili kurejesha huduma ya nishati hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi, Felchesmi
Mramba, ametoa ufafanuzi jana Juni 24, 2014 kuwa baada ya kukatika kwa umeme
saa mbili kasorobo na kuathiri asilimia kubwa ya mikoa yote nchini kukosa
huduma hiyo, ambapo mikoa iliyoathirika zaidi ni mikoa iliyounganishwa katika
gridi ya Taifa na kupelekea kusimama kwa baadhi ya shughuli mbalimbali katika
Taasisi za umma na binafsi ikiwemo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambalo lilikuwa katika zoezi la kupiga kura ya bajeti ya serikali.
Amesema kuwa mafundi wa Shirika hilo waliendelea kufanya
uchunguzi ili kubaini hitilafu hiyo kuwa imesababishwa na kitu gani, na kuweza
kutataua tatizo hilo ambalo limesababisha usumbufu kwa wateja wake.
“Mitambo yetu ya kuzalisha umeme ilizimika ghafla na
inapozimika mitambo kama hiyo inatokana na aidha kuna tatizo au kuna mteja
mkubwa amezima mitambo yake ghafla sasa ilipotokea hivyo na kuzimika kwa nchi
nzima, tulirudisha umeme kwanza ndio tuanze kufuatilia kuwa ninini
kilichopelekea hitilafu hizo”
Aidha, amesema “baada ya umeme kukatika tulichokifanya kwa
haraka sana tulianza kurudisha umme na tulianza na Kituo cha Mtera ambapo
kilipowaka kiliweza kupeleka umeme kwa haraka Dodoma na tuliweza kupeleka pia
mkoani Singida na Mbeya na baada ya hapo kituo cha pili kuwaka ni Kidatu
ambacho kilipeleka umeme mkoani Morogoro na Dar es Salaam na vituo vingine vya
gesi baada ya Kidatu vituo vingine viliwez\a kuwashwa”.
Awali, iliripotiwa katika mtandao wetu kuwa ni fedheha kwa
taifa kukatikiwa na umeme kwa nchi nzima, ambapo baadhi ya wananchi wameonyesha
kutorishishwa na kitendo hicho huku wakitaka viongozi na Mamlaka yenye dhamana
kujiuzulu ili kuondoa aibu iliyoligubika Taifa kwa muda huo.
No comments:
Post a Comment