Katika
wiki chache zilizopita kulikuwa na msuguano kati ya serikali ya Marekani na
China , Serikali ya Marekani inailaumu china kwa kufanya udukuzi kwenye kampuni
zake na biashara nyingine huku china nayo ikiilaumu marekani taarifa juu ya
hili
Uchina
baada ya hali hiyo ikaamua kukataza matumizi ya windows 8 kwenye kompyuta zote
za serikali na taasisi zote zinazopewa fedha na serikali ya nchi hiyo na hili
linaweza kusomeka kwa kirefu na viambatanishi vingine
Serikali
ya China na wataalamu wake kadhaa wanasema matumizi ya windows 8 ni hatari kwa
usalama wao na ustawi wao , kwahiyo wamekataza na kuendelea kutengeneza program
yao ya COS China Operating System kwa ajili ya matumizi ya serikali pamoja na
taasisi zake .
Kwan
nchi za ulaya suala kama hili liliwahi kutokea miaka kadhaa iliyopita , lakini
umoja wa ulaya ulienda mahakamani na mahakama ikaamua Microsoft itoe source
code kwa umoja wa ulaya ili waweze kubadilisha na kuweka mambo yao kwa maslahi
ya umoja wa ulaya .
Kitu
kikubwa ambacho serikali ya uchina inalalamikia kuhusu Windows 8 ni hii source code,
serikali ya china inataka source code ya bidhaa hii ili iweze kuifanyia
mabadiliko iendane na maslahi yake haswa kwenye mambo ya ulinzi na usalama .
Hapa
nchini kwetu tumeona taasisi mbalimbali na wizara mbalimbali za serikali tena
nyeti zikitumia bidhaa mbalimbali za windows bila kufanya mabadiliko yoyote kwa
ajili ya usalama wao , tumeona watu haswa viongozi wakinunua kompyuta na vifaa
vingine vya mawasilino na kuvitumia kuhifadhi taarifa nyeti bila vifaa hivi
kuchunguzwa au kubadilishwa chochote .
Suala
la serikali ya China lituamshe na tuanze harakati za kuangalia maslahi makubwa
ya taifa wakati wa manunuzi na matumizi ya vifaa na program mbalimbali toka
nchi za nje , program hizi na vifaa vyake vinaweza kutumika kwa urahisi
kuhamisha taarifa na chochote kile au kufanya uhalifu bila mnunuzi au mtumiaji
kujua .
Wakati
serikali inafikiria kupeleka muswada wa sheria ya usalama wa mtandao bungeni ,
ni vizuri suala kama hili lijulikana na wataalamu watakaojadili sera au chochote
kinachohusiana na usalama wa Taifa .
Huwezi
kulinda taifa kama taarifa zako zinaweza kuchukuliwa au kuangaliwa na mtu akiwa
popote duniani .
No comments:
Post a Comment