Askari polisi anayelinda usalama wa abiria na mali zao katika kituo cha mabasi yaendayo mikoani akijalibu kutoa maelekezo kwa wanafunzi wa UDOM waliofika kutafuta usafiri kituoni hapo na kukuta hali ya usafiri hailidhishi kutokana na uchache wa Mabasi.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wakigombania kulipa nauli kwa ajenti wa Basi la Urafika linalofanya safari zake kuelekea Iringa baada ya baadhi ya Vyuo kufungwa kwa pamoja na hivyo kufanya idadi ya abiria wa mikoani kuwa wengi kuliko mabasi yaliyopo.
Baadhi ya Abiria wakitafakari na mabegi yao baada ya kufika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani na kujikuta wakikosa usafiri kutokana na uchache wa mabasi ulisababishwa na vyuo vilivyopo mkoani Dodoma kufungwa kwa wakati mmoja.
Na John Banda, Dodoma
DODOMA imekumbwa na uhaba wa usafiri wa mabasi ya kwenda mikoani kutokana na vyuo vikuu na vile vya kawada kufungwa katika kipindi kimoja hali iliyowasababishia abiria usumbufu mkubwa ikiwa ni pamoja
na nauri kupanda kinyemela. Wanafunzi hao hasa wa Vyuo vikuu vya Dodoma (UDOM), Mtakatifu Yohana, Mipango na Maendeleo Vijijini (IRDP) na kile cha Biashara (CBE) ambavyo vina wanafunzi wengi vimefungwa kwa likizo ya miezi mitatu.
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi walipokutwa wamezagaa katika kituo cha mabasi ya kwenda mikoani walisema leo ni siku ya tatu tangu kuusotea usafiri huo bila mafanikio. Neema Binamu alisema kutokana na wanafunzi wa vyuo vyote kukutana kwa pamoja kusaka usafiri imekuwa shida kutokana na Idadi ndogo ya mabasi.
Hali iliyosababisha wenye magari wasiyowaaminifu kupandisha bei kinyemela mpaka kufikia 30,000 badala ya 17000 na wanapolipa kiasi hicho huandikiwa nauri ya kawaida tofauti na hapo hakuna anaesikilizwa.
‘’Kikubwa ni kwa vyombo vinavyohusika na usafirishaji vinatakiwa kujipanga mapema hasa wakati wa misimu kama hii ambayo vyuo vinafungwa ili kutuepushia usumbufu ambao hata hatujui kama tutondoka au la’’,
alisema
Kwa upande wao baadhi ya maajenti ambao hawakutaka kuandikwa majina yao walisema vipindi kama hivi ni vya neema kwao kutokana na siku za kawaida kura dagaa na sasa watakura kuku takribani wiki nzima. Nae Mmoja wa askari wa usalama barabarani aliyekuwepo kituoni hapo alisema yeye si msemaji lakini swala Nauri ya mabasi imegwanyika katika Madaraja matatu ambapo ni 23,000 lile la kwanza na 17,000 la
tatu. Na kuhusu upandishwaji nauri kiholela alisema hilo wanalo na wanawapitia abiria wanaosubili usafiri na kuwapa elimu ili wasilipe zaidi ya nauri iliyowekwa halali.
No comments:
Post a Comment