Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wakiwa na silaha
ya bunduki aina ya SMG na bastola waliokuwa wakitumia pikipiki aina ya sanlg
yenye namba T460 CVQ wamevamia duka la mpesa na kumuua mfanyabiashara Gosbert
Kulwa(59) mkazi wa tambukaleli mjini Geita. Kamanda wa polisi mkoani Geita
Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 11.30 jioni katika
eneo la benki ya NMB ambapo majambazi hao walimpiga risasi ya tumboni
mfanyabiashara huyo wa mpesa na kufariki dunia wakati akipata matibabu katika
hospitali ya wilaya ya Geita.
Amesema mauaji hayo yalifanyika baada ya majambazi hao
kupora kiasi cha pesa ambacho hakijajulikana kutoka kwa mfanyabiashara huyo.
Kamanda ameongeza kuwa kabla hawajamuua Gosbert walianzia
kwenye duka la mfanyabiashara wa vinywaji ndugu Ignas Athanas na walichukua
pesa kiasi ambacho hakijafahamika na
kuchukua bastola aina ya H PIETRO BERRETA HO4788Y CAR 5808 ikiwa na
risasi 12 mali ya mfanyabiashara huyo.
Aidha majambazi hao waliokuwa na bunduki aina ya SMG iliyofutwa
namba zake na risasi 13 na simu ya mkononi aina ya TECNO huku wakiwa wamevalia
makoti meusi na helment ili kuficha sura zao zisitambulike kwa urahisi.
Jeshi la polisi lilipata taarifa muda mfupi zilizotolewa na
raia wema ambapo kamanda wa polisi akiongoza kuwafuatilia majambazi hao
walifanikiwa kuwakuta katika pori lililopo jirani na kijiji cha Ibambila
wilayani Nyangh’hwale zaidi ya km 50 kutoka mjini Geita walipofanya uharifu.
Wakiwa wanakimbizana majambazi hao walipowaona askari
jambazi mmoja aliyekuwa na silaha aliruka kwenye pikipiki na kuanza kuwashambulia askari kwa risasi lakini dereva
wa porisi alimfuta moja kwa moja na kumgonga kwa gari jambazi huyo na kufariki
hapo hapo.
Baada ya hapo jambazi
mwingine alikimbia kwa pikipiki na askari wakaanza kumfukuza wakishirikiana na
wanafunzi wa shule ya sekondari Nyang’hwale na kufanikiwa kumkamata na kuanza
kumshambulia na alifariki wakati anakimbizwa kupelekwa hospitali.
Taharuki hiyo iliyokuwa imeikumba mji wa Geita kwa masaa
takribani 3 kabala hawajakamatwa majira ya saa2 baadhi ya wananchi
wamelipongeza jeshi la polisi kwa kazi waliyoifanya kwa mda mfupi mara baada ya
tukio hilo huku kamanda Konyo akiendelea kuwaasa wananchi wazidi kutoa
ushirikiano kwa jeshi la polisi ili kuimarisha amani katika mkoa huo.
Na Valence Robert-malunde1 blog Geita
No comments:
Post a Comment