Dokta Herman akitahayali baada ya tukio hilo.
Dokta mmoja aliyefahamika kwa jina la Herman amenaswa katika
dispensari moja iliyopo Buguruni Kwamnyamani jijini Dar akijiandaa kumtoa mimba
mwanafunzi.
Awali, kikosi kazi cha kufichua maovu cha (OFM), kilipewa
malalamiko juu ya dispensari hiyo kuwa ni kinara wa mchezo huo mchafu wa
kuwatoa mimba mabinti wadogo hususan wanafunzi wa shule za msingi.
Siku aliyonaswa, ilikuwa majira ya jioni ambapo kaka wa
mwanafunzi (jina tunalihifadhi) aliandaa mtego wa kumnasa daktari huyo baada ya
kupata taarifa kutoka kwa rafiki wa mdogo wake kuhusu mchezo huo mchafu
anaoufanya daktari huyo.
Kaka huyo aliwapigia simu makamanda wa OFM ambapo walitia
timu sambamba na polisi kwenda kuweka ‘kambi’ katika dispensari hiyo
kuhakikisha tukio zima linakuwa ‘recorded’.
Denti huyo akilia.
Kaka huyo alitanguliwa katika dispensari hiyo na kubana
sehemu kumsubiri mdogo wake huyo afike ‘kutoa mimba’ huku makamanda wa OFM
wakiwa wameseti mitambo yao maalum katika kila engo ya eneo hilo.
Majira ya saa tisa, mwanafunzi huyo alifika hapo akiwa
ameongozana na kijana mmoja aliyesetiwa kuwa mpenzi wa mwanafunzi huyo na
kuongea jambo (kumpa fedha) na daktari akiingia chumbani akiongozana na
mwanafunzi huyo huko akiwa na vifaa maalum vya kutolea mimba.
Nesi,dokta chini ya ulinzi.
Baada ya kusubiri kwa dakika tano, kaka wa mwanafunzi huyo
na makamanda wa OFM waliingia katika chumba hicho na kumkuta daktari huyo akiwa
katika pilipilika za kumtoa mimba mwanafunzi huyo ambaye alikuwa amelala chali.
OFM ilifanikiwa kunasa meseji mbalimbali za daktari huyo
zilizokuwa zikielekeza namna ya kufanikisha zoezi hilo la utoaji mimba.
Majirani ambao walishuudia tukio hilo walipongeza sana OFM
kwa kumnasa daktari huyo kutokana na kukithiri kwa tabia hiyo dispensarini hapo.
”Jamani mmefanya vizuri sana kuja kukomesha mchezo huu hapa
tumelalamika sana lakini hatusikilizwi,” alisema mzee mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la mzee Ham
Nesi bibi akijitetea.
Daktari huyo alipelekwa katika kituo kidogo cha polisi cha
Buguruni kisha kuchukuliwa maelezo ili hatua zaidi za kisheria dhidi ya daktari
huyo ziendelee.
Mpaka timu ya OFM inaondoka eneo la tukio hilo, walimuacha
daktari huyo akiwa anashikiliwa kituoni hapo na shauri lake likisomeka
MNY/RB/336/2014.
CHANZO GPL
No comments:
Post a Comment