Bora kuchelewa kuliko kutofika: Divock Origi akifunga bao lake la ushidni zikiwa zimesalia dakika 2 mpira kumalizika.
MCHEZAJI kinda aliyetokea benchi, Divock Origi ameifungia bao pekee Ubelgiji ikishinda 1-0 dhidi ya Urusi usiku huu katika mchezo wa kombe la dunia.
Haikuwa rahisi kwa Ubelgiji kupata matokeo, lakini zikiwa zimesalia dakika mbili mpira kumalizika, kinda huyo mwenye miaka 19 alifunga bao muhimu akimalizia kazi nzuri ya Eden Hazard.
Ushindi huo umewafanya Ubelgiji kuongoza kundi H kwa kujikusanyia pointi 6 na kwa maana hiyo wameshafuzu hatua ya 16.
Kikosi cha Urusi: Akinfeev, Kozlov, Ignashevich, Kanunnikov, Glushakov, Kokorin, Berezutskiy, Shatov, Samedov, Fayzulin, Kombarov
No comments:
Post a Comment