Mbunge wa jimbo la Kalenga mkoani Iringa Godfrey Mgimwa akitumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura wake katika kijiji cha Kivalali kata ya Ifunda baada ya gari lake kupata pacha wakati wa zikara hiyo hivyo kulazimika kutafuta baiskeli ili kufika haraka mkutanoni kusikiliza kero za wananchi wake ,amini ni mbunge wa kwanza mkoa wa Iringa kutumia usafiri kama huu kuwafikia wananchi wake,picha nyingine akisalimianana wananchi wa kijiji Kivalali (picha na Francis Godwin Blog)
Na Francis Godwin, Iringa
MBUNGE wa jimbo la Kalenga Godfrey Mgimwa amevunja rekodi ya wabunge wa jimbo hilo na majimbo mengine ya mkoa wa Iringa na Tanzania kwa kuachana na matumizi ya magari ya kifahari na kuamua kutumia usafiri wa Baiskeli kuwatembelea wapiga kura wake.
Huku wananchi wa kata ya Ifunda na Mgama wakisema kuwa ubunge wa Mgimwa si wa mwaka mmoja ama mitano bali hadi mwaka 2025 hadi mwenyewe atakavyo sema yatosha .
Mbunge Mgimwa atumia usafiri wa Baiskeli kuwafikia wapiga kura ,wao wasema hawahitaji mbunge mwingine hadi 2025
Mbunge huyo alifikia hatua hiyo jana baada ya mmoja kati ya magari yake mawilio yaliyokuwa katika msafara wake kukwama kulazimika kutumia usafiri huo wakati wa ziara yake ya siku mbili ya kuwatembelea wapiga kura wake na kupokea changamoto mbali mbali
Alisema kuwa amelazuimika kuumia usafii huo ili kuwafikia wananchi wake kwa wakati kutokana na gari lake kupata tatizo japo aliasema usafiri huo ni wa kawaida kwani amekuwa akiutuimia toka utoto wake na kuwa kazi ya ubunge si kujitenga na wananchi bali kuwa karibu nao kwa mazingira ambayo wao wamekuwa wakiishi .
Mgimwa alisema kuwa katika ubunge wakle kamwe hatajitenga na wananchi wake na badala yake ataendelea kuwa karibu nao kwa kuishi kama wao wanavyo ishi ili kujua changamoto zao badala ya kutumia usafiri wa magari kila wakati .
Alisema kuwa si kawaida kwqa mbunge kutumia usafiri huo wa Baiskeli ila kwa kuwa yeye ni mwakilishi wa wananchi ni lazima kuwa tayari kutumia usafiri wowote kulingana na mazingira na kuwa kamwe wana Kalenga wasitegemee kuwa walikosea kumpa ubunge ila wanapaswa kuendelea kujivunia kwa kumchagua kuwa mbunge wao kwani ni nafasi ambayo anaipenda na kamwe hatawaangusha katika kuwatumikia .
Japo aliwataka wana kalenga kuepumka kubadili wabunge kama nguo zao kwani kufanya hivyo ni kujirudisha nyuma katika maendeleo na kuwataka kujifunza kutoka katika majimbo ambayo wabnunge wake wameongoza kwa zaidi ya vipindi vitatu na maendeleo yameonekana .
Pia alisema kuwa huu si wakati wa wana kalenga kuwakumbatia wale ambao wanajipitisha kutaka kuungwa mkono mwaka 2015 na badala yake wanapaswa kuwachukia watu hao na kuwaogopa kama ugonjwa wa ukoma kwani fedha wanazotoa kwa sasa ni fedha ambazo wanawakopesha kwa riba kuibwa ya kutaka ubunge ili kurudisha fedha hizo na sio kuwatumikia wananchi.
Mwisho
No comments:
Post a Comment