Aliingia kumaliza kazi!:
Memphis Depay akitokea benchi amefunga bao la tatu kwa shuti la mbali na
kuipa ushindi wa mabao 3-2 Uholanzi.HATA kama Louis van Gaal alianza kufunga,
lakini haikuwa mechi ya kukaa kwenye kiti. Ulikuwa mchezo mgumu kwake kutokana
na uimara wa Australia, lakini dakika za mwisho zimemalizika kwa Uholanzi
kushinda mabao 3-2.
Bao la kusawazisha alilofunga Timu Cahil liliwashitua
Waholanzi ambao waliokuwa wanashangilia bao la Arjen Robben, lakini kabla
hawajakaa wakashangaa nyavu zao kutikishwa.
Australia ambao wako kiwango cha chini kuliko timu zote
zinazoshiriki kombe la dunia mwaka huu, walifanya shambulizi la kushitukiza na
kufunga goli bora. Pia walijiamini, walikuwa na mipango na kuwayumbisha wana
fainali hao wa 2010 nchini Afrika kusini na wababe wa mabingwa Hispania katika
mchezo wa kwanza ambao walishinda mabao 5-1.Bao la kwanza la Uholanzi
lilifungwa na Arjen Robben, lakini Australia wakasawazisha kupitia kwa Tim
Cahil.
Autralia waliandika bao la kuongoza kupitia kwa Mile Jedinak
kwa mkwaju wa penati, lakini Robin Van Persie aliisawazishia Uholanzi na
hatimaye Memphis Depay akitokea benchi alifunga bao la tatu na la ushindi.
Mlinda mlango wa
Australia, Matthew Ryan
akiangalia mpira uliopigwa na Depay na kuzama kimiani.
Mshambuliaji wa Manchester United , Van Persie akishangilia bao lake la tatu katika
fainali za mwaka huu za kombe la dunia.
|
No comments:
Post a Comment