Kitu cha pili kambani:
Ivan Perisic (wa pili kulia)akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao
la pili.
KITENDO cha Alex Song kumfanyia madhambi mshambuliaji wa
Croatia, Mario Mandzukic na kuoneshwa kadi nyekundu rasmi kimeua matumaini ya
Cameroon kufuzu hatua ya 16 ya kombe la dunia katika kundi A mjini mjini
Manaus.Song alishikwa na hasira dakika ya 40 na kufanya kitendo cha kinyama kwa
Mandzukic wakati huo Cameroon ikiwa nyuma kwa bao 1-0.
Baada ya Hispania kutupwa nje ya michuano, Cameroon imekuwa
nchi ya kwanza kwa Afrika kufangasha virago katika fainali za kombe la dunia
mwaka huu kutokana na kipigo kikubwa cha mabao 4-0 dhidi ya Croatia.
Kufuatia kadi
nyekundu ya Song, mambo yalikwenda kombo zaidi na kushuhudia Cameroon
wakimalizia usiku vibaya baada ya kufungwa mabao matatu kipindi cha pili na
ndoto za kufuzu kuzimwa kabisa.
Hata hivyo kituko kikubwa ni beki wa Tottenham Benoit
Assou-Ekotto kuamua kupigana na mwenzake
Benjamin Moukandjo katika hatua za
mwisho za mchezo huo.
Assou-Ekotto na Moukandjo wakitunishiana misuli baada ya kutofautiana
Chukua kichwaaa hichooo dogooooo usilete maneno tena sawaaaa
Ahhhhh wewe unampiga nani?Moukandjo akimkaba Assou-Ekotto baada ya kupigwa
unazingua sanaa weweeeee akissema Moukandjo
Samuel etoo akimtulizaaaa Assou-Ekotto baada ya kutaka kurudi kupigana tena
Etooo niachieee yule dogo mbishii nikamfunze adabuuu
No comments:
Post a Comment