Wamiliki wa mtandao wa kijamii wa Facebook ambao una
watumiaji wengi zaidi duniani wamelazimika kutoa maelezo juu ya kuondoka hewani
kwa mtandao huo kwa muda wa dakika 30 dunia nzima.
Msemaji wa Facebook amenukuliwa akisema kuwa “Mapema leo
asubuhi tulipata tatizo kubwa la watu kushindwa kuingia na kuandika chochote au
kupost picha katika mtandao wetu kwa muda wa dakika 30″
Anaendelea kwa kusema kuwa wametatua tatizo hilo haraka na
kufanikiwa kurejesha mtandao huo hewani kwa asilimia 100 ambapo pia ameomba
radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
No comments:
Post a Comment