U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.
Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.
WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Mara nyingi wanawake ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.
No comments:
Post a Comment