Watu watatu wamekufa na wengine kumi wamejeruhiwa baada ya
gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noha kupasuka tairi ya nyuma na kubingirita
mara tatu katika kijiji cha Januka manispaa ya Singida.
Akithibitisha kitokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa
hospitali ya mkoa wa Singida daktari Deogratias Banuba amesema wamepokea maiti
mbili wakiwa wamesha fariki eneo la tukio akiwemo dereva wa Noha bwana Enock
Mbaga, binti Ajira Juma na maiti nyingine ya Bi Tatu Bunku ambaye alikuwa herd
mistres Ngimu sekondari amefia katika hospitali ya mkoa wa Singida .
Daktari Banubasi amesema majeruhi kumi wamepatiwa
huduma ya kushonwa sehemu mbalimbali za miili yao na wanaendelea
na matibabu ,pia hakuna majeruhi ambaye atapatiwa rufaa .
Mmoja wa majeruhi akiongea kwa shida huku akiwa amelazwa
katika hospitali ya mkoa wa Singida bwana Ramadhani Mlenga amesema gari
halikuwa katika mwendo wa kasi na gafla likaacha njia na kupinduka mara tatu.
No comments:
Post a Comment