Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya wajasiriamali wa sekta isiyo rasmi ya Jumuhiya ya Afrika Mashariki; yajulikanayo kama Nguvu Kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kufanyika Kigali Rwanda,Novemba 30 hadi Desemba 7 mwaka huu. Kulia ni Afisa Kazi Mwandamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Sara Daudi.Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wajasirimali Tanzania, Joseph Rweyemamu (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano na waandishi wa habari, leo jijini Dar e s Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza 30 hadi Desemba 7 mwaka huu. Kushoto ni Afisa Kazi Mwandamizi wa Wizara ya Kazi na Ajira, Sara Daudi.Mratibu wa Chama cha Utabibu wa Dawa Asili Tanzania, Boniverntura Ferdinand (katika), akiwaeleza umuhimu wa dawa asilia wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam kuhusu maonesho ya 15 ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yajulikanayo kama Nguvu kazi/Jua Kali yanayotarajiwa kuanza Novemba 30 hadi Desemba 7 mwaka huu, kulia ni Afisa Habari Mkuu wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema na kushoto ni Mweka Hazina wa Shirikisho la Vyama vya Wajasiriamali Tanzania, Jumbe Ngutto. Picha na Lorietha(Laurence-Maelezo)
WAZIRI JAFO ATAKA HUDUMA KWA WAKATI ZAHANATI YA BWAMA.
-
Waziri wa Viwanda na Biashara na Mbunge wa Jimbo la Kisarawe Mhe.
Dkt.Selemani Jafo(Mb) amemtaka Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe
kuhakikisha huduma ya...
6 hours ago
No comments:
Post a Comment