David Cameron amesema amejutia kumuajiri kama mshauri wake
Aliyekuwa mhariri wa gazeti moja nchini Uingereza Andy
Coulson ambaye baadaye alihudumu kama mshauri wa waziri mkuu wa Uingereza David
Cameron amehukumiwa kifungo cha miezi 18 gerezani kwa makosa ya udukuzi wa
mawasilioni ya simu.
Wiki iliyopita Coulson alipatikana na hatia ya kudukuwa
mawasiliono ya simu alipokuwa mhariri wa gazeti la News of the World.
Gazeti hilo baadaye lilifungwa kutokakana na shinikizo
kutoka kwa umma nchini Uingereza kufuatia kashfa hiyo ambapo simu za famiia za
kifalme, za wanasiasa, za watu mashuhuri na watu wa kawaida zilidukuliwa.Kufutia
hukumu hiyo, waziri mkuu wa Uingereza aliomba msamaha kwa kumteua Coulson kuwa
mshauri wake.
Waandishi wengine wa zamani na mchunguzi wa kibinafsi Glenn
Mulcaier walikiri kufanya udukuzi wa mawasiliono ya simu na walipewa hukumu
ndogo.
CHANZO BBC
No comments:
Post a Comment