Msanii Dogo Janja ambae aliondokaTiptop kwa kishindo na
kufanya kazi na Ustaz Juma na Musoma, amerejea tena kambini (Tiptop) baada ya
kuona maisha ya mtaani ni magumu
Akielezea kurudi kwake ndani ya Tiptop Madee amesema
"Mi nilipigiwa simu na babu tale pamoja na Fela kwamba
Abduli amekuja, kama miezi miwili imepita, amekuja anasema mkae myamalize, mi
nikawaambiwa aah mbona mi sina tatizo, kwasababu mi mbona naongea nae,
kwasababu akiwa na tatizo lake ananitumia meseji ananiomba ushauri, sema tu kwa
maswala hayo ya kazi sijawahi kuongea nae chochote.
kuna siku alifanya interview namillard alisema. alitubu
mambo aliyokuwa anayaongea kwamba ulikuwa ni utoto, na kweli mi nikaangalia kwa
haraka haraka umri aliokuwa nao mwanzo na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.
jana pia nikakuta hizo taarifa nikawaambia mbona mi sina
tatizo, tukamuita maskani jana tukaongea nae fresh, basi mpaka sasa hivi tuko
nae, lakini bado hakuna vitu vingi vinavyoendelea, bado mapema sana,
tukishakuwa tayari tutawaambia, lakini ukweli ni kwamba Abduli, Dogo Janja
amejoin tena kwenye connection yetu , hicho ndio cha msingi, mengine yote
tutawapa taarifa"
Dogo Janja pia nae pia alifunguka sababu za kurudi tena
kwenye kambi yake aya mwanzo
"kwasababu kwanza kuna vitu ambavyo namiss katika mziki
wangu na pia nimemiss familia yangu ya mwanzo, kuna vitu ambavyo vinamiss
katika mziki wangu hata watu wangu wanaona, nakuwa niko tofauti sana na
mazingira ya mziki, sawa naweza kuwa na record sana lakini nyimbo naweka ndani
tu, lakini tofauti na huku unapangiwa labda utatoa ngoma hii uutatoa ngoma hii
hivyo tu"
kuhusu yeye na Ostaz Juma na Musoma
"Mkataba tu uliisha, tuko poa ila mkataba wangu mi na
yeye uliisha, tuko fresh" amesema Dogo Janja
No comments:
Post a Comment