Mhe. Omar Mjenga, leo amepata fursa ya kuitembelea kampuni ya
Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai, kwa
lengo la kujionea miradi mikubwa iliyotekelezwa na kampuni hiyo.
Baadhi
ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai
(the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart
na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.
Kufuatia
mazungumzo kati ya Mhe. Mjenga na Bw. Rashid Lootah, mwenyekiti wa
NAKHEEL, wamekubaliana kwa pamoja kuwa mwenyekiti huyo na ujumbe wa
washauri na wataalam wake kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania,
tarehe 10 hadi 13 Agosti, 2014.
Wakiongozana na
Mhe. Balozi Mdogo Mjenga, watakutana na taasisi mbali mbali zikiwamo
NHC, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), TTB, TANAPA na zingine nyingi.
Aidha, watapata fursa ya kuongea na Mawaziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Viwanda na Biashara, Ardhi,
Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Kampuni
hiu ina nia ya kuwekeza katika hotel za nyota tano, nyumba za makazi na
biashara pamoja na maduka makubwa(shopping malls).
|
No comments:
Post a Comment