Balozi wa Libya nchini Tanzania amejiua kwa kujipiga risasi
kichwani.
Mwandishi wa BBC mjini Dar es Salaam , John Solombi anasema
kuwa balozi huyo kwa jina Ismail Nwairat, alijipiga risasi Jumanne usiku na
kufariki akiwa anapokea matibabu hospitalini.
Msemaji wa serikali ya Tanzania Arthur Mwambene
amethibitisha taarifa hiyo kuwa balozi huyo alijiua ndani ya makao ya ubalozi
wa Libya mjini Dar es Salaam Jumanne usiku.
No comments:
Post a Comment